EXCLUSIVE (TANZANIA) – Radio hazifanyi usawa katika upigaji wa muziki wa wasanii – Peter Msechu

 

Msanii aliyetoa single yake mpya ya ‘Malava’ hivi karibuni, Peter Msechu amelalamikia hali iliyopo katika vyombo vya habari na kudai ndio chanzo cha nyimbo nzuri kutopata nafasi ya kufanya vizuri katika soko la muziki.

Alikiambia kipindi cha Jump Off cha Times FM, Msechu amesema alikuwa akijaribu mara kwa mara kufanya ‘nyimbo’ nzuri kwa maendeleo ya Bongo Flava lakini hazieleweki zinapoishia.

“Nafikiri kuwe na utaratibu mzuri redioni, kuwe na usawa katika upigaji wa nyimbo”, alisema. “Sasa kama mmoja atalia mara moja alafu mwingine akalia mara kumi tutakuwa tunafelishana tu, Ifike kipindi tupewe nafasi sawa alafu kizuri kijiuze wananchi wenyewe waamue. Kuna mambo lazima tuyaache” aliongeza Peter.

Leave your comment