EXCLUSIVE (TANZANIA)- Kiba atoa utata wa post yake aliyoiweka Instagram

 

 

Msanii Ali Kiba ametolea ufafanuzi post yake aliyoiweka Instagram ambapo ilileta hisia tofauti kwa mashabiki mbalimbali wa muziki.

Tarehe 16 Novemba Kiba aliweka post iliyosomeka “Asanteni sana najua mmepiga kura sana lakini nilikuja kugundua baada ya kufuatilia kuwa kuna mambo yanaendelea ya watu wanadiriki hata kupoteza pesa zao kwa ajili yangu ila nawaomba fans msinielewe vibaya I will always be there for you #hapakazitu #KingKiba”, na baadae post hiyo aliifuta.

Katika kipindi cha Ala Za Roho cha Clouds FM na Diva The Bawse, King Kiba alisema watu walimuelewa vibaya na ndio ilikuwa sababu kubwa ya yeye kuifuta post hiyo.

“watu walinielewa vibaya mimi nilikuwa nawaambia mafans wangu, sababu wao ndio walinipigia kura sikumaanisha kuhusu tuzo walinielewa vibaya”,alisema Kiba.

Japokuwa yeye hakuweza kushinda kipengele hata kimoja kati ya vinne alivyotajwa kuwania katika tuzo za AFRIMA 2015, lakini hakumpongeza msanii hata mmoja wa Tanzania aliyeshinda ambao ni Vanessa na Diamond, kutokana na hilo Ali alisema;

“Siwezi ku-post kitu kuhusu kushinda kwao, unajua hakuna uzalendo. Watu wangapi wanafanya vitu vizuri hawapongezwi? Mimi nafanya vingapi? Sisi sio wazalendo… Unajua watu mimi hawanijui wanahisi kama naringa hivi au nina wivu, ila mimi nawapenda wasanii wote pia mziki mzuri” aliongeza Ali Kiba.

Na alipoulizwa uhusiano wake na Diamond akasema wako vizuri, na kumpongeza kwa ushindi wa tuzo alizoshinda.

Leave your comment