EXCLUSIVE (TANZANIA)- Ali Kiba akonga nyoyo za mashabiki Kenya kwenye Koroga Festival
17 November 2015

Siku chache zimepita tangu msanii Ali Kiba alipotumbuiza mbele ya mastaa wa Hollywood katika hafla ya Wild Aid jijini Los Angelos, Marekani. Wikiend iliyoisha Kiba alitumbuiza katika tamasha la Koroga Festival jijini Nairobi, Kenya.
Msanii huyo aliyekuwa na bendi yake alifanya show matata iliyosifiwa na maelfu ya wapenzi wa muziki huku akiwapa mashabiki wa kike kile wakipendacho kwa kuwaonesha kifua chake cha mazoezi.
Wakati akitumbuiza wimbo wa mwana Kiba alichana vest yake nyeusi na kuonesha kifua chake na kuwaacha warembo wakipiga kelele.




Leave your comment