EXCLUSIVE (TANZANIA) – Ommy Dimpoz ajibu swali la Wolper “Kwanini wanamuziki wa Tanzania hutumia models wa nje”?
13 November 2015

Siku kadhaa zilizopita Jackline Wolper aliuliza kwanini wanamuziki wa Tanzania hawatumii models wa kitanzania na kutumia wa nje ya nchi. Ommy Dimpoz ambaye amefanya video zake kadhaa nje ya nchi aeleza sababu.
Kupitia kipindi cha Planet Bongo cha East Afrika Radio Ommy alisema “Mara nyingi models wa nje wako professional wanaweza kucheza character zote ambazo wamepangiwa”.
“huku unajua kidogo kuna scene ambazo mtu anatakiwa acheze lets say amevaa swimming costume, unajua huku kumpata msichana ambaye anayejiachia hivyo ni wachache sana, hata kama ikitokea mnaweza mkajikuta msichana huyo huyo anatokea kwenye video za watu wote” aliongeza Dimpoz.
Pia Ommy aliongeza sababu ya kupunguza gharama ya watu wa kusafiri nao, kwasababu husafiri na dancers wao kwenda kushoot video nje na kwa nje ukilipia video inamaana umelipia kila kitu,ikiwa ni pamoja na models.
Hata hivyo models kwa nje wanapatikana kwa bei rahisi na hivyo husaidia kupunguza gharama.
Siku chache zilizopita msanii wa Bongo Movie Jackline Wolper aliuliza kupitia Instagram, kwanini wasanii wetu wote wanatumia zaidi models wa nje kwenye video zao. Bila shaka Ommy Dimpoz atakua amejibu swali lake.




Leave your comment