NEW RELEASE (TANZANIA) – Peter Msechu- Malava Malava
13 November 2015

Msanii Peter Msechu anatarajia kuachia wimbo mpya unaitwa Malava Malava. Kupitia ukurasa wa Instagram ametoa taarifa kwa mashabiki kuhusu ujio wa wimbo wake mpya.
Aliandika “Its official my next song will be out next week…#MALAVA
Produced by @teazvillah
Written by @barnabaclassic & @petermsechu
#MALAVA #MALAVA #MALAVA #MALAVA #MALAVA #MALAVA
STAY TUNED…………….!!!!!!!!!!!
Wimbo huo umetengenezwa na Teaz Villah na kuandikwa na Barnaba pamoja na Peter Msechu mwenyewe. Peter Msechu aliwahi kushiriki katika shindano la Bongo Star Search la Tanzania mwaka 2009 na baadae kushiriki Tusker Project Fame iliyokuwa inahusisha Afrika Mashariki nzima na kushika nafasi ya pili.
Peter mpaka sasa anatamba na kibao cha Relax alichomshirikisha Kidumu wa Burundi, na nyimbo zake nyingine nyingi kama Nyota akiwa na Amini, Unaniumiza, Kumbe na zingine nyingi.




Leave your comment