EXCLUSIVE (TANZANIA)-Alikiba atumbuiza kwenye hafla ya WildAid huko Marekani
12 November 2015

Weekend iliyopita shirika la WildAid lilifanya hafla ya kwanza ya ukusanyaji wa fedha jijini Los Angeles, Marekani na kufanikiwa kukusanya dola milioni 2.5.
Hafla hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya Montage Beverly Hills, na kupewa jina la “An evening in Africa” na kuhudhuriwa na mastaa kibao wa Hollywood, Ali Kiba alitumbuiza.
Kati ya mastaa waliohudhuria ni Maggie Q maarufu kupitia series ya Nikita na muimbaji wa zamani wa kundi la Black Eyed Peas na mume wake Josh Duhamel, Kristin Bauer na Diane Warren. Ambapo bendi za kiafrika zilitumbuiza na dance, pia alipata nafasi ya kupiga picha na mastaa waliohudhuria.
Pia AliKiba alishare kupitia ukurasa wake wa Instagram picha za yeye na mastaa hao na kuandika “Was Amazing Weekend@fergie @Wildaid #wildaidambassadors”.
“Nikita @maggieq_1 Nilifurahi Kumuona @Wildaid #wildaidambassadors”.




Leave your comment