EXCLUSIVE (TANZANIA)- Lollypop naye kuwania tuzo za Extreem Kenya

 

Mwimbaji, mtunzi wa nyimbo na mtayarishaji muziki kutoka Tanzania Goodluck Gozbert anaefahamika kama Lollypop ametajwa kuwania tuzo za muziki wa injili nchili Kenya.

Tuzo za Xtreem ni  kubwa zinazofuatia baada ya Groove Awards na zimeendeshwa kwa miaka miwili.

Mwanamuziki huyo anayefanya muziki wa injili na pia ameandika mashairi ya wimbo wa Basi nenda wa Mo Music na Siachani Nawe wa Baraka De Prince. Ambapo alipatia jina kwa kupitia utunzi wake mzuri wa nyimbo.

Lollypop alitajwa kuwania katika kipengele cha wimbo bora na msanii bora kutoka Tanzania.

“Ilikua kama surprise kujikuta katika tuzo za Extreem kwasababu kwanza sikuweza kufikiria kama muziki huu ninaoufanya ndani ya Tanzania unaweza kuwa tayari umeshavuka mipaka ndani ya muda mfupi hivi” alisema Gozbert.

Pia alisema kuwa wimbo wa ‘Acha Waambiane' ndio uliomuwezesha kutengeneza aina ya muziki ambayo itakuwa inavuka mipaka ya nje ya Tanzania. Na kuongeza kuwa kutajwa katika kuwania tuzo hizo za Extreem ni fursa kubwa kwake na wakati sahihi wa kuvuka mipaka.

“Ziko namna tofauti za kuweza kunipigia kura na hii inategemea zaidi na mpiga kura wapi na ni kwa namna gani anaweza kuwa na urahisi wa kunipigia kura. Watu wa Extreem Awards wameweka upigaji wa kura kupitia mitandao ya kijamii ambayo ili kunipigia kura unaingia kwenye page zao na kucomment XT 229 Goodluck Gozbert”

Kwa kufanya hivyo utakuwa tayari umeshapiga kura ambapo page ya Facebook ni Xtreem Awards, Instagram: @xtreemawards na Twitter @xtreemawards2015.

Source:Bongo 5

Leave your comment