EXCLUSIVE (TANZANIA)- Q-Chief kufunga ndoa January 2016
9 November 2015

Mwanamuziki maarufu nchini Abubakar Shaaban a.k.a Q- Chief au Q Chilla ambaye tayari amefanikiwa kuwa baba wa mtoto mmoja yupo mbioni kuuacha ubachela.
Msanii huyo ametangaza kuwa kwa sasa ameona ni wakati muafaka wa kufunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu.
Akizungumza na E-News ya EATV, Q Chief amesema katika maandalizi yake hayo ya harusi itakayofanyika mwezi January mwakani, pia ameandaa wimbo maalumu kwa ajili ya mchumba wake huyo ambaye ni mzaliwa wa hapa Tanzania.
“Wimbo ambao nimemzawadia mke wangu mtarajiwa ambaye natarajia kumuoa January katikati hapo, ni mwanamke mstahimilivu ambaye amenipa moyo katika kipindi kigumu kwahiyo nikasema hapana ngoja nifanye kitu kwa niaba yake kwahiyo hii ni zawadi yake” alisema Q-Chilla.




Leave your comment