EXCLUSIVE (TANZANIA)- King Kiba kufanya kazi na Choreographer wa Rihanna,Chriss Brown, Ne-yo, Nicki Minaj,Ciara.
5 November 2015

Ali Kiba atafanya kazi na mwalimu maarufu wa dance na ambaye CV yake ipo vizuri wa Marekani, Oththan Bumside, aliyetoa taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Choreographer huyo aliweka picha ya mwanamuziki Ali Kiba anyetamba na kibao cha “Chekecha” na kuandika “Excited to be working with @officialalikiba #EastAfrica #KingKiba your in great hands! #OtheezyCreatedIt#CreativeDirector #Choreograph S/O @msaagency @Brandonlouisla!!! #MSAFAM thank you guys”.
Ali Kiba alijibu, “Excited to be working with you too. See you in a bit”.
Mpaka sasa haijajulikana Kiba atamtumia Choreographer huyo katika nyimbo gani lakini ni wazi kuwa kazi hiyo itakuwa nzuri na yenye kiwango kikubwa itakayofanyika nchini Marekani. CV ya Bumside ni nzuri, kwakuwa ameshawaelekeza kucheza wasanii wakubwa wa Marekani kwa ajili ya video zao ama ziara za muziki.
Kati ya video za muziki alizoelekeza jinsi ya kucheza ni pamoja na Believer ya Keysha Cole, Champion ya Mila J, Come With Me ya Ne-Yo, Loyal ya Chriss Brown, I got it ya Ashanti ft Rick Ross, Turn It Up ya Rihanna, Love More ya Chriss Brown ft Nick Minaj, Boyfriend ya Justin Bieber na nyingine nyingi.
Pia amezunguka kwenye ziara kubwa za wasanii kama co-choreographer zikiwemo Rihanna (Diamond World Tour), Ciara (Jackie Tour), Miley Cyrus (Bangerz Tour), Usher (OMG Tour) na nyingine nyingi.
Pia alishiriki kuelekeza dance ya kwenye tuzo nyingi za Marekani zikiwemo za BET Awards, MTV Awards na zingine.
Katika upande wa filamu Bumside pia alishiriki kuelekeza Stomp the Yard (2007) na School Dance(2014). Bumside anafanya kazi chini ya kampuni ya MSA Agency.




Leave your comment