EXCLUSIVE (TANZANIA)- Thamani yangu na muziki wangu ni kubwa kuliko tuzo- Ali Kiba

 

Msanii Ali Kiba ameweka wazi jinsi gani anvyozichukulia tuzo katika kazi yake ya muziki au kama zinamwongezea thamani yoyote.

Mwimbaji huyo wa “Chekecha” ambaye huwa haudhurii kwenye tuzo nyingi ikiwemo na zile ambazo pia huibuka mshindi, ameeleza ni kwasababu gani huwa haudhurii.

“Nimegundua  kwamba mimi ni mwanamuziki ambaye si focus sana kwenye tuzo ameiambia AYOTV. Lakini kiukweli muziki wangu una thamani kubwa na mimi ni mkubwa zaidi ya tuzo, kwahiyo kunapokuwa kama hakuna ulazima nafanya biashara yangu” alisema Ali Kiba.

Wizkid pia ni kati ya wasanii wakubwa kutoka Afrika ambaye hajali sana kuhusu tuzo, hata pale anapotangazwa kuwania huwa hajishughulishi sana kuomba mashabiki wampigie kura na huwa haimsumbui kwa kutokuwa na tuzo nyingi. Na alisema huwa anafanya mambo makubwa kuliko hizo tuzo na ndio maana huwa hajishughulishi sana.   

Leave your comment