EXCLUSIVE (TANZANIA)- Dully ataja nyimbo atakazofanyoa shooting nje ya nchi
4 November 2015

Msanii wa Bongo Fleva Dully Sykes azitaja nyimbo zake alizopanga kufanyia shooting nje ya nchi. Mwimbaji huyo mkongwe ambaye hakuwahi kushoot video nje kabla amesema kwa sasa anafikiria kufanya hivyo kwa nyimbo ambazo amewashirikisha wasanii wa hapa nyumbani wakiwemo ambao tayari wameanza kujitangaza kimataifa.
Dully alisema kupitia 255 ya XXL,“Nina nyimbo na wasanii kama Vanessa Mdee, Diamond Platnumz, Christian Bella na Mzee Yusuph. Sifikirii hizi kama nitafanya hapa Tanzania, nawezakutoka”.
Dully ambaye ametoka kuachia wimbo mpya Dodoma ameongeza kuwa ana wimbo mwingine aliowashirikisha Yamoto Band waliouandika. Amedai hakuweza kushoot video nje kwasababu ni wimbo unaohitaji mandhari ya nyumbani.
“Tungeweza kwenda nje lakini nyimbo ambayo tumeimba na Yamoto haikubase huko kwenye kiu-nje nje. Imekuwa ni ya Kiswahili sana, na sifikirii kama tungeweza kupata magenge huko nyanya nini, tusingeweza kupata na ndio maana tumeamua kufanyia hapa Temeke”.aliongeza Dully.




Leave your comment