EXCLUSIVE (TANZANIA)- Wizkid kuahidi show ya bure baada ya mapokezi mazuri

Msanii wa Nigeria Wizkid aahidi show ya bure baada ya kupewa mapokezi mazito toka kwa mashabiki wa Tanzania, na kughairi safari yake ya kurudi Jijini Lagos.

Msanii huyo alioneshwa kushangazwa na shangwe za mashabiki wakati akifanya show, hali iliyomfanya atumbuize kwa muda mrefu zaidi stejini. Alisema hajawahi kukutana na mashabiki wenye upendo kuwazidi watanzania.

“Ilikua niondoke lakini sitoondoka na kesho natafuta sehemu nikutane tena na nyie, tufanye concert ya bure” alisema wizkid.

“Nimefurahi sana kuona hali hii, Tanzania mna upendo wa kweli. Tuendelee kuwa pamoja nami kwenye twitter na Instagram ili tujue tunakutana katika ukumbi gani” alisema.

Bahati mbaya jumapili hii Wizkid alishindwa kupata kibali na kuandika katika ukurasa wake wa Instagram,

“Last night in Dar es Salaam, Tanzania!! Had to jump on the speakers to be close to my people! Love u all. Unfortunately, we couldn’t get the permit to do the free concert today but I’m coming back in December! Fiesta moves!!!!! Yaaaaaa!!!

Pia aliipongeza Tanzania kwa kumaliza uchaguzi salama. 

Leave your comment