EXCLUSIVE (TANZANIA)- Barnaba kumrejesha Najma kwenye muziki
29 October 2015

Msanii na mmiliki wa studio za High Table Sound Barnaba boy ni mtu mchakarikaji na ni mtunzi mahiri wa mashairi ya muziki. Licha ya kumiliki studio pia ameanzisha label na bendi yake, huku akiendelea kufanya kitu anachokipenda zaidi cha kuandika nyimbo.
Kati ya watu wanaotarajia kunufaika na kipaji chake ni muimbaji Naj ambaye miaka ya hivi karibuni alipotea kwenye game. Wawili hao wameingia studio usiku wa kuankia jumatano hii na kurekodi ngoma ya pamoja kwenye studio hizo.
Barnaba alipost picha kwenye ukurasa wake wa istagram na kuandika “Hello Tanzania we out here working with the beautiful @najdattan”
Nae Naj alipost picha hiyo na kuandika:@ the studio @hightablestudio kwa chief @barnabaclassic now.
Naj aliwahi kutamba na single inayoitwa Don’t Let Me Go akimshirikisha Mr Blue. Pia aliwahi kushirikishwa na Fid Q kwenye wimbo wake wa Swagga Don.




Leave your comment