EXCLUSIVE (TANZANIA)- Video ya Collabo ya Diamond na Ne-Yo kufanyika Marekani na Afrika
29 October 2015

Diamond Platnumz ambaye amefanya kolabo na msanii mkubwa wa RnB Marekani, ameelezea mahali ilipofikia project hiyo inayotarajiwa kumfungulia milango ya mafanikio zaidi kimataifa.
Akizungumza na mtangazaji wa Citizen Kenya, Mzazi Willy Tuva, Diamond amesema wimbo huo umekamilika lakini hawezi kusema utatoka lini kwa sasa kuna baadhi ya mambo ambayo anayaweka sawa kabla ya kuachia.
Platnumz ambaye wiki iliyopita aliibuka mshindi wa tuzo za MTV EMA kipengele cha ‘Best Worldwide Act Africa/India’, amesema anafikiria kufanya shooting ya video hiyo Marekani pamoja na Afrika.
Ne-Yo ambaye alikutana na kufanya kazi na Diamond wakati wa CokestudioAfrika jijini Nairobi, Kenya alikua miongoni ya watu waliompongeza Baba Tiffah kwa ushindi wa tuzo ya MTV EMA kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika “CONGRATS TO MY HOMMIE @diamondplatnumz for winning #BestWorldWideAct at MTVEMA’s keep being great! lets go get them my guy!”




Leave your comment