EXCLUSIVE (TANZANIA)- Msanii Barnaba aanzisha bendi yake (Barnaba Classic)
28 October 2015

Mtunzi, mwimbaji na mtayarishaji wa muziki Barnaba ameanzisha bendi yake mwenyewe. Msanii huyo aliiambia tovuti ya Bongo5 bendi yake ilikuwepo ila kwa sasa itakuwa na vifaa vya kisasa.
“Nina bendi toka muda mrefu ila sasa hivi ndo naifanya kuwa official. Naanza kununua vifaa vyangu vya muziki au kama mtu akitokea akaninunulia sio mbaya pia” alisema.
“Bendi itakuwa ni bendi tofauti na zingine zote unazozijua. Mimi sitopiga kama wengine kwenye maukumbi, sitafanya hivyo. Bendi yangu itakuwa kwa shughuli maalumu, kwenye sherehe kubwa, matukio yoyote makubwa itakuwa inafanya”aliongeza Barnaba.
Source:Bongo5




Leave your comment