EXCLUSIVE(TANZANIA)- Diamond Platnumz ashinda tuzo za MTV EMA “Best World Wide Act Africa/India".

Msanii Diamond amezidi kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kwa mara nyingine, kwa kushinda tuzo kubwa ya “Best Worldwide Act Afrika/India” katika tuzo za MTV Europe Awards 2015 zilizotolewa Milan, Italy usiku wa Jumapili Oktoba 25.

Hii ni kwa mara ya kwanza kwenye historia ya tuzo za MTV EMA toka vipengele vya Worldwide Act vilipoongezwa kwenye tuzo hizo mwaka 2011, tuzo ya  “Best Worldwide Act Afrika/India”imekuja Africa mwaka huu.

Diamond ambaye pia alishinda kipengele cha “ Best African Act” kwenye tuzo hizo, alikua akichuana na mwigizaji na mwimbaji maarufu wa India, Priyanka Chopra aliyewahi kuwa Miss World mwaka 2000.

Ushindi wa Diamond ni mkubwa kwasababu hakuwa anaiwakilisha Tanzania pekee bali bara la Afrika kwa ujumla.

Hii ndiyo list ya washindi waliowahi kushinda kipengele alichoshinda Diamond mwaka huu,

2011-Abdelfrattah Grini (Morocco)

2012- Ahmed Soultan (Morocco)

2013- Ahmed Soultan (Morocco)

2014- Mohamed Assaf (Palestina).

Leave your comment