EXCLUSIVE (TANZANIA)- Badilisha Poetry X-change ipo njiani kuja Tanzania

 

Je una kipaji au uwezo wa kuandika mashairi? Hii ndiyo nafasi yako mtanzania ya kuonesha kipaji chako cha uandishi wa mashairi au malenga. Taasisi ya Africa Centre kupitia mradi wao wa  Badilisha Poetry X-change wanakupa nafasu ya kukuza kipaji chako cha ushairi. Waandishi wanaweza kuwasilisha mashairi yao kwa maneno au katika mfumo wa sauti kwa kuingiza katika website yao inayonekana pichani.

Badilisha X-Change ni maktaba kubwa katika mtandao wa mashairi ya kiafrika duniani kote. Afrika centre inatembelea majiji mbalimbali barani Afrika kurekodi kazi ya ushairi kwa ajili ya maktaba hiyo. Waratibu wa taasisi hiyo wanatarajia kuja jijini Dar es salaam kwa ajili ya kazi hiyo. Ili kuangalia baadhi ya mashairi kutoka Tanzania yaliyowasilishwa hadi sasa kwa kufuata link hii Tanzania|Badilisha Poetry –Pan-African Poets.

Leave your comment