EXCLUSIVE (TZ) – Abdu Kiba ‘AYAYA’ ilibidi nifanye na Vanessa ila ikashindikana
20 October 2015

Msanii Abdu Kiba asema nyimbo yake ya Ayaya aliyoifanya na Rubby ilibidi afanye na Vanessa Mdee ila haikuwezekana. Mwanamuziki huyo ameiambia Siz Kitaa ya Clouds FM kuwa Vanessa alimuacha njia panda kwa muda mrefu bila kujibu ndio maana akafanya na Rubby.
“kwanza nili-plan kufanya wimbo na Vanessa, nilimtumia ule wimbo wakati umetimia wote kwasababu niliweza kuutunga wote, akausikia ila ilishindikana kufanya kwasababu process zake zilikua nyingi” alisema “ kwanza alikuwa busy na kazi zake, mara ana safari ya kwenda nje ya nchi, so na mimi time ilikua inanibana, mashabiki wanahitaji kazi kutoka kwangu kwahiyo nikaona kwanini nimsubiri wakati nina deni kwa mashabiki! Baada ya kuona Vanessa hana jibu analonipa mimi nikaona nimtumie Rubby aweze kuusikia kwasababu kuna mistari ambayo niliiweka na ilikuwa inastahili mtoto wa kike aimbe” aliongeza Abdu Kiba.




Leave your comment