EXCLUSIVE (TANZANIA): 'Never Ever' Yagharimu Zaidi Ya Dolla 20,000!

Msanii Vanessa aliyetoa video hivi karibuni ya wimbo unaoenda kwa jina la Never ever, amesema video imemgharimu zaidi ya dola 20,000 ambayo ni sawa na Millioni 40 za kitanzania.

Video ilifanyika nchini Afrika Kusini chini ya Director Justin Compos. Kwa mujibu wa mtandao wa Clouds FM Vanessa alisema “Video ya wimbo wangu wa Never Ever imenigharimu dolla elfu 20 sawa na millioni 40 za Kitanzania nimefanya kwa producer Justin Compos, na malengo yangu bado sana hata sijafika ukurasa wa pili wa kitabu ninachoandika na matumaini ya kuvuka mipaka mingi Zaidi”


Mwanadada huyo anayefanya vizuri katika game la muziki Tanzania na Afrika kwa ujumla, anatamba na vibao vingine kama Game, Hawajui na Come over.

Leave your comment

Top stories