Bongo Flava: Umoto Wa Mnanda Wa Diamond Platnumz “Moyo”

[Image Source: Instagram]


Writer: Elizabeth Betha


Download Kamba Dj Mixes On Mdundo

Msanii mashuhuri kutoka kiwanda cha muziki Tanzania, Nasibu Abdul almaarufu Diamond Platnumz aka Simba ameachia wimbo wake mpya kwa mwaka huu alioupa jina la Nifanyaje, miondoko ya wimbo huu ni tofauti na ngoma alizoziachia hivi karibuni ambazo nyingi zilikuwa na mahadhi ya Amapiano na Bongofleva kidogo.

Nifanyaje iko katika mahadhi ya aina ya muziki unaojulikana kama Mnanda ambao unakaribiana kidogo na Singeli, na kwa upi ulianza basi ni Mnanda ndioulianza halafu ikaja Singeli. Ni aina ya muziki ulio maarufu sana katika mitaa ya Uswahilini ama kwa Waswahili halisi. Diamond ameonesha uwezo mkubwa wa kupita kwenye mdundo na ni kama ameshafanya aina huu ya muziki kwa muda mrefu kwa jinsi alivyoweza kuuvaa na kuachia muziki mzuri.

Haina ubishi kwamba ni moja ya kazi zake bora na amezidi kuonesha uwezo wa kuimba aina tofauti za muziki, inawezekana ni namna ambavyo Simba ni msanii anaethubutu kufanya muziki wa aina yoyote na kwa umaarufu wake ulimwenguni inasaida kuweka kwenye ramani muziki wa nyumbani kama Mnanda.

Humo ndani stori kubwa ni kuumizwa kwenye mapenzi na mahusiano, jambo ambalo Diamond analiwezea sana kwani ana hits za kutosha zinazohusiana na mapenzi zinazoendelea kufanya vizuri hata sasa. Kwenye Nifanyaje Diamond ameimba;- 

“Siwezi sema kitandani, labda umasikini wangu

Ndio kilionishusha thamani, wathaminike wenzangu

Siwezi sema sikujali, labda vizawadi vyangu mimi

Havikufikia ukubwa, wanavyotoa wenzangu

Kinachoniumza, ridhiki hugawa Mola

Ingelikua mimi, mbona angehomola

Na mbaya zaidi, rafiki wananichora

Kwa hizo post zake, na wenye nguvu la dollar

Uwooh!

Oooh mi moyo wangu mama

Unaona uchungu

Mwenzake mi moyo wangu, anaaumiza sana

Sema nitafanya nini, ndo hivyo nitafanyaje

Ila nitafanya nini, ndo hivyo nitafanyaje”

Ungetamani kuendelea kuona wasanii wengine wakiachia nyimbo za aina hii ya muziki, share maoni yako kwenye sehemu ya maoni ili twende sawa. Usiache kusambaza upendo Valentine’s hii.

 

Leave your comment