Mtoko Wa Valentine’s Ya Aslam Tz
13 February 2025
[Image Source: Instagram]
Writer: Elizabeth Betha
Download Kamba Dj Mixes On Mdundo
Unamfahamu kama Aslam TZ lakini jina lake halisi ni Ally Masoud Ally, ni msanii wa muziki wa kizazi kipya kutokea Dar es Salaam, Tanzania. Kwa muda mfupi ameweza kujikusanyia kijiji chake cha mashabiki wanaoukubali muziki wake, na haina ubishi mwamba anajua sana.
Kwa mujibu wa bio yake anaweza kufanya muziki wa aina tofauti ikiwemo Bongofleva, Zuku, Afro Pop, Amapiano na nyingine. Amejiwekea misingi mizuri iliyojaa utaratibu na kujiheshimu kutokana na makuzi na Imani yake yake ya kidini. Vyote hivi vinaonesha kuwa Aslam ni msanii wa kuangaliwa kwani uwezo anao na tunaweza kuamini na kutegemea mazuri zaidi kutoka kwake.
Hana muda mrefu sana kwenye tasnia, lakini toka ameanza hata sasa kuna utofauti unaopimika kutokana na kuongezeka kwa ubora wa kazi zake kadiri siki zinavyoenda, kwa maana kwamba kazi yake ya kwanza haifanani na ya pili au ya tatu na kadhahalika, kwasababu ameendelea kuongeza viwango katika kwenye kitu kama uimbaji, maudhui, midundo, video nk, hii inaonesha kuwa anapenda anachokifanya na anajali mashabiki zake kwa kuwapa kazi nzuri kila anapoachia.
Aslam ana nyimbo za kutosha kuhusu mambo ya mapenzi na mahusiano, na katika msimu huu wa wapendanao amehakikisha hukosi cha kusikiliza na umpendae au hata mwenyewe kulingana na hali yako ya mahusiano. Nyimbo zake kama Namuota, Raha, Hanipendi Tena, Wakuniliza, Turudiane, Moyo ni baadhi ya kazi zake bora.
Akiwa anafunga mwaka 2024, aliachia goma la kufungia mwaka alilolipa jina Tukutane Mwakani ambayo aliitolea remix yake akiwa na Masauti kutoka Kenya na Mabantu ni moja ya kazi nzuri zilitufungia mwaka na mpaka sasa inaendelea kufanya vizuri. Mwaka huu hajaanza kinyonge, kwani hivi karibuni ameachia wimbo wake mpya alioupa jina Asante akiwa na Barnaba Classic aka Mopao, ni kazi znuri sana ukizingatia amemshirikisha fundi kwenye muziki.
Tuendelee kumsapoti Aslam TZ kwasababu anajua na kwa jinsi ameanza mwaka huu basi yajayo yanafurahisha zaidi. Share kwenye uwanja wa comments wimbo wako pendwa kutoka kwake na tuendelee kusambaziana maupendo Valentine’s hii.
Leave your comment