Za Moto Kwenye Mdundo Januari Hii!

[Image Source: Instagram]


Writer: Elizabeth Betha


Download Kamba Dj Mixes On Mdundo

Mwaka mpya wa 2025 haujaanza kinyonge kwenye tasnia ya muziki kwani wasanii wameachia kazi zao za kutosha mwezi huu na kifupi ni kwamba burudani iliyopatikana ni ya kutosha, na ni wazi mwaka huu utakuwa mkubwa na mzuri kwa wasanii na tasnia kwa ujumla kwani kazi zilizotolewa kwa mwezi huu wa kwanza zibashiri hayo na zaidi.

Msanii kutoka label ya Kings Music, Vanillah ameachia kazi yake mpya aliyoipa jina ya Najikubali. Humo ndani kawashirikisha Chino Kidd na Tommy Flavour, haina ubishi kwamba goma ni la kwenda na ujumbe ni mzuri kwa mashabiki zake na wapenzi wa muziki kwa ujumla kwani ni  kama anawakumbusha umuhimu wa kujiamini binafsi kwanza halafu ndo wengine nao watakuamini ama kukubali. Moja ya kionjo kikali kwenye wimbo huo ni pale Vanillah ameimba;-

Asante Muumba, huna baya wewe

Watu wanakunja, unanipa wewe.

Ukitembelea tovuti ya mdundo.com utaipata burudani hiyo bila kukwama, kwani ni ya moto kabisa kwako wewe na wapenzi wa muziki wote popote Tanzania na hata nje ya Tanzania.

Rapcha TZ nae ana wimbo mpya kabisa alioupa jina la Dangerous Desire, kama ilivyo kawaida yake, Rapcha ni muhadithiaji mzuri sana kwenye nyimbo zake na hii kazi haina tofauti zaidi tu ni kwamba ni kali na ujumbe wake ni mzuri sana, hususani kwa wadada wanajitafuta kwenye maisha. Humo ndani Rapcha ameimba;-

Hii ni kwa ninayemuona kwenye kioo, mwisho wa kuogopa ndio maisha yanapoanza

Giza hutoweka siku mpya inapoanza, inuka hapo ulipo anza!

Ubunifu, tungi na midundo iliyotumika kutengeneza kazi hiyo imefanikiwa kwa asilima kubwa kuifanya iwe kazi nzuri sana kutoka kwake Rapcha. Hii pia unaipata ukitembelea tovuti ya mdundo.com, hapo unaweza kupakua na kuisikiliza bila kukwama kwama.

 

Tovuti ya ndundo.com ipo kukuhakikishia unapata burudani ya muziki wa nyumbani na kwingineko bila tatizo, popote ulipo Tanzania, tembelea leo uienjoy muziki mzuri na watu wako wa nguvu. 

 

Leave your comment