Kubadilisha Upepo Wa Muziki Anjella Tz

[Image Source: Instagram]


Writer: Elizabeth Betha

Download Kamba Dj Mixes On Mdundo

Tukiwa mbioni kuingia mwaka mpya msanii wa muziki wa kizazi kipya Anjella TZ, alitangaza kuachana na muziki wa Bongofleva na kurudi madhababuni kwa Mungu. Kwa wengi tafsiri ya haraka ni kwamba Anjella ana uwezekano wa kuanza kuimba nyimbo za Injili na kumtumikia Mungu kupitia huko.

Anjella ni mwanadada mwenye kipaji na sauti nzuri sana ya uiambaji na ni wazi kazi zake zote ambazo alishazitoa zinajieleza uwezo alionao. Aliingia rasmi kwenye tasnia baada ya kutambulishwa kama msanii katika ‘label’ ya Kondegang yake Harmoize, na tangia hapo safari yake ya muziki ikaanza.

Miaka ya karibuni aliweza kutoka chini ya ‘label’ hiyo na kuwa msanii huru, huku akiendelea kufanya muziki na kutumbuiza kwenye matamasha mbalimbali Tanzania. Na hivi karibuni baada ya kupitia changamoto kadhaa aliweza kushikwa mkono na msanii mwenzie Zuchu kwa kukabidhiwa gari kwaajili ya kumrahisihia kazi zake kama msanii.

Na hivi karibuni ndio ametangaza kuachana na muziki wa Bongofleva, na kwa uelewa wa haraka anatarajia kufanya muziki wa Injili japokuwa hajatangaza rasmi.

Kwa hapa Tanzania wasanii wengi tu waliweza na wao kubadilisha upepo wa kimuziki kutoka huku kwenda huku, na kwa mada hii wasanii ambao walihamia kwenye muziki wa Injili kutoka kwenye Bongofleva ni kama Stara Thomas, Walter Chilambo, Bella Kombo nk. Wote wanafanya vizuri sana kwenye muziki wa Injili wakijizolea mashabiki ndani na nje ya Tanzania.

Kila mmoja wao akiwa ana sababu zake za kuhama, lakini jambo moja la wazi ni kwamba mashabiki zao na wapenda muziki wanabarikiwa sana na kazi zao wanazozifanya, na kama ambavyo Bongofleva ina mashabiki wengi vivyo hivyo muziki wa Injili wa Tanzania una mashabiki wengi, na hiyo haijifichi kupotia tovuti za muziki, matamasha na views huko Youtube nk.

Hivyo Anjella ana uwezo wa kufanikiwa zaidi kwenye muziki wa Injili, kwakuwa tayari ana mashabiki zake binafsi lakini pia kipaji anacho cha kutosha hivyo hamna cha kumzuia kufikia malengo yake huku akiwa anamtumikia Mungu, tutegemee makubwa kutoka kwa Anjella TZ.

Leave your comment