Ubunifu Kwenye 'Blessings' Kusah

[Image Source: Instagram]


Writer: Elizabeth Betha
Download Kamba Dj Mixes On Mdundo

Kusah aka Brow ameachia ngoma yake mpya aliyoipa jina la Blessings. Inaweza kuchukuliwa kama ngoma ya kufungulia mwaka, kwa maana ya maudhui yake na ujumbe mzima uliopo humo ndani.

Mpaka sasa wimbo una siku chache tu, lakini mapokeo yake ni mazuri sana na hii ni kwasababu ya ubunifu mzuri unaoutumika kuipromote hio kazi nzuri iliyofanyika. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kusah ameweza kutumia maudhui mbalimbali na kuwatumia watoto wake ambao nao tayari wanajulikana na mashabiki zake kusaidia kupamba hizo video zake huko Instagram.

Wimbo kwa ujumla unabeba ujumbe wa kuwa na matumamini ya kufurahia mwaka mpya, kwa kuhakikisha mtu anatimiza malengo yake na ikiwezekana kuvuka malengo huku akiwa anafurahia mwaka mzima yeye pamoja na watu wake wa karibu. 

Tumezoea kuona nyimbo za kufunga mwaka na kutarajia mwaka unaokuja, lakini kwa Kusah ameamua kutu’bless’ na wimbo wa Blessings kwenye mwaka mpya kabisa. Ameachia video kadhaa akiwa na watoto wake, na Dj Tammy nk, zote zikiwa na lengo la kuwapa mashabiki zake na wapenzi wa muziki mzuri, ladha inayopatikana kwenye wimbo wake mpya kabisa.

Kusah ni msanii anaendelea kuonesha bidi kila iitwapo leo, na popote utakapomsikia iwe kwenye nyimbo zake mwenyewe ama akiwa ameshirikishwa na wasanii wenzie, ameendelea kuhakikisha mashabiki zake wanapata burudani safi ya viwango kwakuwa hana kazi mbovu.

Soko la muziki linavyozidi kukua ndivyo na wasanii wanamakinika kuhakikisha wanawafikia mashabiki wa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania, hii yote ni ili ulimwenguni kote kuwepo na mashabiki wa muziki wa nyumbani. Kwenye wimbo huu Kusah katumia lugha za Kiingereza na Kiswahili na ni wazi itasaidia kushika si tu mashabiki wa hapa nyumbani lakini hata nje ya Tanzania. 

Kama Kusah anavyoimba ni mwaka wa Blessings nyingi sana kwetu sote, basi iwe hivyo na kuzidi! Share hapo kwenye comments mstari uliokuvutia zaidi kwenye wimbo wa Brow aka Kusah.

https://www.youtube.com/watch?v=UR0CSF-c1FA

Leave your comment