Muziki wa Mwaka 2025…
8 January 2025
[Image Source: Instagram]
Writer: Elizabeth Betha
Download Kamba Dj Mixes On Mdundo
Takribani miaka mitatu au zaidi hadi sasa aina ya muziki wan je uliteka soko la muziki wa hapa kwetu Tanzania. Hapa nazungumzia muziki kutoka kwa Madiba (Afrika ya Kusini), Amapiano. Mpaka sasa wasanii karibia wote ambao wako kileleni wana ngoma zaidi ya moja zenye miondoko ya Amapiano na kufanya aina nyingine ya muziki kuzaliwa inyoijulikana kama Bongopiano, na ni kwasababu kinachotumiaka hapo ni miondoko ya wenzetu lakini lugha inyotawala ni Kiswahili.
Katika kipindi chote hicho mashabiki na wapenzi wa muziki mzuri wameburudishwa na nyimbo mbalimbali za miondoko hiyo na penye ukweli usemwe, wasanii wa Bongo wameweza kutoa ‘hit’ za kutosha za Bongopiano ambazo hadi leo zinafanya vizuri.
Lakini tukirudi katika asili ya kinyumbani, muziki uliokuwa umeteka soko kwa muda mrefu ni Bongofleva yenyewe na ilhali wasanii wengi walikuwa wanatoa nyimbo nyingi za Bongopiano, bado muziki wa kwetu uliendelea kupenya kupitia kazi mbalimbali za wasanii kama Jay Melody, Ali Kiba, Nandy, Zuchu, Phina, Marioo nk.
Kwa upande mwingine muziki aina ya Singeli nao uliendelea kupenya kati ya miondoko hiyo mengine, kwa wasanii kama Dulla Makabila, Meja Kunta, na wengine kutoa nyimbo zao. Lakini pia mwishoni mwa mwaka tumepata kollabo ya Singeli kati ya Meja Kunta na Ibraah inayojulikana kama Gang Gang, ila pia ngoma ya Singeli ya mwaka jana inayotwa Wivu, yote hii inaonesha kuwa ilhali soko la muziki kwa asilimia kubwa limetekwa na Bongopiano lakini aina nyingine za muziki wa nyumbani nazo ziko vizuri na mashabiki wanazipokea.
Tumeanza mwaka mpya siku kadhaa tu, na uelekeo unaenda kubadilika kwa minajili ya kwamba, wasanii wameonesha kutaka kurudi kwenye asili yao yaani Bongofleva, lakini pia kufanya muziki wa Singeli kwa sana, ambao ukipewa nafasi ni muziki unaoweza kutuwakilisha kimataifa zaidi.
Lakini pia kwa mtazamo wa ubunifu kuna aina tofauti za muziki wasanii wetu wanaweza kuzitumia kubadilisha ladha. Mwaka 2025 muziki unaenda kubadilika kwa namna ya tofauti, kwasababu wasanii wameonesha kuamka na hasira zaidi katika kukuza hadhi zao hivyo tutegemee muziki mzuri zaidi wa miaka yote.
Leave your comment