Stamina : 'Albamu Bora Ya Hip Hop" Na Matokeo Yake
17 December 2024
[Image Source: Instagram]
Writer: Elizabeth Betha
Download Kamba Dj Mixes On Mdundo
Msanii Stamina Showrebwenzi ameendelea kutikisa na ujio wa albamu yake aliyoiachia mwezi uliopita katika siku yake ya kuzaliwa tarehe 14 Novemba, Stamina ambaye ni msanii wa miondoko ya Hip Hop ama kwa Kiswahili rahisi muziki wa kufoka foka/michano ameweza kuachia moja ya kazi bora kwa mwaka huu wa 2024.
Albamu yake inayojulikana kama Msanii Bora wa Hip Hop ni albamu iliyobeba uzito wa kutosha kwa maana kuanzia utaaraishaji, mashairi, ‘features’ na ubinifu uliotumika humo umeweza kuifanya albamu yake kupokelewa vizuri na mashabiki zake na hata wadau wa muziki Tanzania.
Stamina amezungumzia vitu mbalimbali katika albamu hiyo yenye nyimbo 17 ambazo kabla ya kuizindua hakuwahi kuachia hata mkwaju mmoja, hivyo kuifanya albamu yake kusubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki zake na wana Hip Hop kwa ujumla. Likija suala la ‘features’ humo ndani ameweza kushirikisha wasanii wa ‘caliber’ zote kwa mantiki ya kwamba wasanii ambao walikuwa kwenye tasnia tangia zamani kama Stara Thomas, Ferooz, Linah, Mwasiti, Marlaw, Belle 9 na wengine, na humo ndani pia kuna wasanii chipukizi ambao ndio wanaanza safari ya muziki na Stamina ameweza kuwapa shavu kuwepo kwenye albamu yake. Lakini pia amevuka mipaka ya Tanzania na kushirikisha wasanii kutoka Afrika Mashariki akiwemo Bface kutoka Burundi.
Mpaka sasa albamu inapatikana katika tovuti zote za kupakua na kusikiliza muziki ikiwemo Mdundo, na tukipima kwa matokeo ya albamu yanaonesha kuwa imepokelewa vizuri, kwa maana watu wanaisikiliza sana na wameikubali hivyo hata namba za usikilizaji na utazamaji zinabashiri ubora na mapokeo yake mazuri kwa watu.
Stamina hivi karibuni alitangaza kupitia ukurasa wake wa Instagram,kuwa amejipanga kuifanyia ‘promotion’ albamu yake kupitia kutumbuiza katika mikoa mbalimbali hapa Tanzania. Safari ya kwanza ilikuwa ni kwenye mkoa wa Dodoma ambako huko alisindikizwa na baadhi ya wasanii aliowashirikisha kwenye albamu yake ya Msanii Bora wa Hip Hop na wengine walioamua kumuonesha tu upendo, wasanii walioenda nae ni Pamoja na Linah, Belle 9, One Six, Marlaw, TID na FAMA.
Albamu ya Msanii Bora wa Hip Hop imeonesha kufanikiwa kwa kipindi kifupi toka kuzinduliwa kwake, na kwa jinsi wasanii wenzake na mashabiki kwa ujumla wanavyoendelea kuipeleka mjini, ni wazi kuwa itaendelea kufanya vizuri.
Kati nyimbo 17 za kwenye Msanii Bora wa Hip Hop ipi ni track kali zaidi kwako ambayo unaisikiliza mara kwa mara? Share kwenye comments hapo na mwambie mwanao na mwanao amwambie mwanae asiache kuisikiliza albamu ya Stamina kupitia mdundo.com
Leave your comment