“Itakuwaje” Kollabo Ya Ushindi Kwenye Sama Ep
2 December 2024
[Image Source: Instagram]
Writer: Elizabeth Betha
Download Kamba Dj Mixes On Mdundo
Queen wa Bongo RnB Maua Sama siku kadhaa nyuma aliachia ngoma yake mpya akiwa amemshirikisha Ali Kiba, almaarufu King Kiba, na jina la wimbo ni “Itakuwaje” ambayo ni track namba 2 kwenye EP yake mpya inayoitwa SAMA.
Nimeiita kollabo ya ushindi kwasababu King Kiba na Maua Sama wote ni wakali, nyimbo hii ina hadhi ya bongoflava ya zamani ya kubemebelezana, na sauti zao kwa pamoja ni burudani tosha hususani kwa mashabiki wa Sama na Kiba. Hii ni mara ya pili wakali hawa kushirikiana, mara ya kwanza ikiwa miaka miwili iliyopita walipotoa “Nioneshe” ambayo nayo ilikuwa kollabo kali.
Hadi sasa wimbo huu umeendelea kujipatia umaarufu japokuwa bado hajaachia video yake, lakini umeenda mjini na mapokezi ni mazuri. Mashabiki wa Maua Sama na Ali Kiba waliipokea kollabo hii vizuri na matokeo yanaonekana kupitia idadi ya views zilizopatikana kwa kipindi kifupi toka uachiwe. Comments za mashabiki wa muziki mzuri nazo hazikuwa mbali kupongeza ufundi uliooneshwa kwenye kollabo hii kati ya wakali hawa.
Mpaka sasa ameachia tu audio ya wimbo huo katika chaneli yake ya Youtube na hadi sasa imefikisha views 157k ambayo ni namba nzuri ukizingatia ni wiki 2 tu toka auachie
Kwa mujibu wa Maua Sama wimbo huu umejaa furaha, shauku na vibes nzuri za mapenzi, mtu yoyote akisikiliza anaenjoy na mpenzi wake. Wimbo wa “Itakuwaje” ni wimbo namba 2 kwenye EP ya Maua Sama ambaye hivi karibuni pia aliachia Bongopiano yake inayoitwa “Kariakoo”, humo ndani kawashirikisha Ibraah, Jaivah na G-Nako na huo wimbo ni track namba 4 kwenye EP yake hiyo hiyo ya SAMA.
Kollabo hii ya Ali Kiba na Maua Sama inatazamiwa kuleta ladha tofauti na ushindani mkubwa kwenye nyimbo za miondoko ya taratibu zilizotolewa na wasanii tofauti miezi hii ya karibuni. Wimbo huu unakusudia kukupeleka kwenye safari nzuri ya mahaba na uhakika kusikia hali ya mapenzi ikitawala kila ukisikiliza.
Wimbo huu pia unategemewa kutengeneza challenge nyingi za kuimba sana sana kwasababu ya muundo wake na jumbe iliyotolewa humo. Maua anakukaribisha kusikiliza wimbo wake mpya kupitia chaneli yake ya Youtube kwa kubonyeza link iliyopo hapo chini.
Mpaka sasa umeshasikiliza kollabo ya ushindi? Umeipokeaje na ungependa kusikiliza na nani mkiwa wapi? Share majibu yako hapo chini kwenye sehemu ya comments.
Leave your comment