Sherehe Ya Kiwanda Cha Burudani Na Mdundo Tanzania

[Image Source: Instagram]


Writer: Elizabeth Betha


Download Kamba Dj Mixes On Mdundo

Tarehe 21 Novemba ilikuwa siku maalumu kwa Mdundo Tanzania lakini pia wadau wa muziki wa Tanzania kwa uwepo wa Tanzania Industry Stakeholders Event ikiwa na lengo la kukutanisha wasanii wa muziki Tanzania, wadau wa muziki kwa maana ya waandishi wa habari, taasisi za fedha na wapenzi wa muziki walikusanyika kwa Pamoja kujadili mustakabali wa soko laz muziki Tanzania na namna tunaweza kuzivuka changamoto zilizopo ili wasanii wafaidike na sanaa yao lakini pia kufika anga za kimataifa.

Mshereheshaji wa siku Bi. Khalila Mbowe alinogesha shughuli nzima kwa kuhakikisha wahudhuriaji wanashiriki kikamilifu kwenye mijadala lakini pia kuchangamsha kwa maswali yaliyohusiana na muziki wa nyumbani, ni wazi walioweza kufika ni wapenzi wa muziki kwa jinsi waliweza kujibu kwa uharaka na uchangamfu maswali mbalimbali yaliyoulizwa.

Mgeni rasmi alitakiwa kuwa Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Hamis Mwinjuma, lakini hakuweza kufika hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Mdundo Tanzania Bi. Maureen Njeri aliweza kusimamia muongozo wa shughuli nzima.

Bi. Maureen Njeri alielezea historia ya Mdundo Tanzania, nini haswa inafanya kwa muziki wa Tanzania na bidhaa za muziki zizazopatikana Mdundo, alitambulisha timu ya Mdundo ya Tanzania na vitu gani wanafanya, pia alidokeza kuwepo mazuri yanayokuja kupitia ushiriakiano kati ya Mdundo na Foundation ya benki ya CRDB. Ushirikiano huo unategemewa kuleta mageuzi makubwa kwa tasnia ya muziki.

Majadiliano kamili yalianza wakati jopo la wataalamu na wadau wa muziki wa Tanzania walipoweza kupata nafasi ya kuzungumzia mustakabali wa soko la muziki Tanzania na vitu vya kurekebisha ili muziki wetu kukuwa zaidi. Jopo liliongozwa na mshereheshaji wa siku Bi. Khalila Mbowe na wanajopo ni pamoja na Amani Martin ambaye ni Meneja wa Masoko na Ubinifu wa benki ya NMB, Emmanuel Kiondo ambaye ni Mkuu wa Masuala ya Kampuni kutoka CRDB, Fido Mgaigai ambaye ni mtaarishaji, msanii na mtangazaji wa muziki wa Singeli, Benedicto Anthony ambaye ni Mtangazaji na Mkuu wa Idara ya Digitali kutoka Crown Media, Bi. Lucy Tomeka kutoka Mwananchi Communication Limited.

Masuala mbalimbali yaliweza kuzungumziwa lakini machache ya muhimu yalityoiliwa mkazo, ni suala la wasanii kufikisha jumbe zao kwa kutumia lugha nzuri isiyo na maneno yasiyo sawa, jambo hili lilisitizwa haswa na Bw. Fido Mgaigai ambaye anafanya kazi na wasanii hususani wa Singeli kwa ukaribu sana, lengo ikiwa waweze kuteka soko la ndani na la nje ya Tanzania, lakini pia alisistiza kuupa muziki wa Singeli nafasi na tuuamini kama ni muziki wa heshima na wakutufikisha anga za kimataifa.

 

Jambo jingine liliopewa uzito ni umuhimu wa wasanii kujizingatia hususani linapokuja suala la kukuza chapa zao (brand) kwa minajili ya kwamba wakijichukulia kawaida ndivyo watu wengine watakavyowachukulia, na wakiweza kuwekeza kwenye vitu vya kukuza hadhi zao basi wataweza kupata heshima na nafasi wanazostahili kuzipata, suala hili lilitiliwa mkazo na Bw. Benedicto Anthony lakini pia Bw. Amani Martin ambao wote wameweza kufanya kazi kwa ukaribu na wasanii wa muziki.

 

Bw. Kiondo ambaye ni mtaalamu wa masuala ya fedha alisisitiza umuhimu wa wasanii kupata elimu ya fedha,  ili kuweza kuepuka kuishiwa pale tu wanapoapata changamoto hususani wakiwa wameshuka kimuziki. Alitumia nafasi yake kusisitiza umuhimu wa wasanii kuwekeza kwenye muziki wao kwa kufikiria wakati wa mbele, kwa kuwa na bima, kununua hisa na kuwekeza kwenye miradi ambayo itakayoendelea kuwapa kipato hata ikitokea soko lao la muziki likishuka kwa wakati fulani. Wasanii ni vioo vya jamii na wamekuwa ni sehemu ya kufikisha ujumbe kwa jamii kuhusu masuala ya fedha, lakini hali si shwari kwao binafsi hivyo Bw. Kiondo alitoa rai kwa taasisi za fedha kuwapa elimu ya fedha wasanii wetu wa Tanzania.

 

Uwepo wa tukio hili umeweka nuru mpya kwa tasnia ya muziki Tanzania na ni wazi kwamba yanayokuja mbele yatawafaidisha wasanii na wadau wa muziki Tanzania ili kila mmoja wao aweze kufanikiwa kupitia sanaa yao kimuziki lakini pia kiuchumi wawe katika nafasi nzuri. 

 

Tukio zima lilifana na burudani ilikuwa ya kutosha na wahudhuriaji walipata nafasi ya kusabahiana na kujadiliana masuala muhimu kwaajili ya tasnia ya muziki,  itoshe kusema yajayo yanafurahisha.

https://mdundo.com/song/3427541 

Leave your comment

Top stories