Hiphop ya zamani VS hip hop ya sasa

Hip hop nchini Tanzania imepitia mageuzi makubwa kutoka mizizi yake ya zamani hadi sauti za kisasa. Wasanii kama Mr. II (Sugu) na Professor Jay walizungumzia masuala ya kijamii kama umasikini na ufisadi. Muziki wao ulikuwa na ujumbe mzito – ni kama walikuwa wakisoma taarifa ya habari lakini kwa beats pamoja na vina vikali. Huwezi kuongelea hip hop ya zamani bila kumtaja Mangwair, ambaye alijulikana kwa mtindo wake wa kipekee na mashairi yenye nguvu, aliweza kuunganisha vijana wengi kupitia muziki wake. Wanamuziki hawa waliweza kuchanganya sauti za kitamaduni za Tanzania na beats za hip hop ya Marekani, wakifanya utambulisho wa "utamaduni wetu" uonekane kuvutia kwa washabiki wa muziki.

Wasanii wa sasa kama Rosa Ree, Roma Mkatoliki, Kontawa, Bill Nass, na Joh Makini wanachanganya mitindo kama Bongo Flava na trap. Rosa Ree, anayejulikana kwa sauti yake kali na ujasiri wa kuzungumza masuala ya kijamii na ya kibinafsi, ameweza kuleta mabadiliko makubwa katika muziki wa hip hop. Bill Nass, kwa upande mwingine, ana mtindo wa kipekee unaochanganya nyimbo za upendo na maisha ya kila siku, akileta ladha mpya kwenye muziki wa kisasa. Roma Mkatoliki anajulikana kwa mashairi yake yenye nguvu na ujumbe wa kijamii unaochochea fikra, huku Kontawa akiweka upekee kwa kuchanganya hip hop na ladha za kisasa za muziki wa dunia. Joh Makini, anayejulikana kwa uandishi wake wa kipekee na uwezo wake wa kuchambua masuala ya kijamii na kisiasa, ameongeza kina katika muziki wa kisasa wa hip hop. Matumizi ya teknolojia ya kisasa na vifaa vya studio vya hali ya juu yameboresha sauti na utofauti wa muziki wa kisasa. Mitandao ya kijamii kama Instagram na YouTube imewawezesha wasanii kufikia mashabiki wengi zaidi kwa haraka ukilinganisha na wasanii za zamani.

Katika kusherehekea miaka 51 ya Hiphop nchini, tunawaletea DJ mix maalum yenye nyimbo za hip hop ya zamani na ya kisasa ili kuonyesha safari hii ya muziki. Sikiliza mix hii kujionea utofauti kati ya hip hop ya zamani na hii ya sasa kupitia :https://mdundo.ws/youngLunya

Leave your comment