Ngoma Mpya: Jaivah Aimarisha Ufalme Wake Kwenye Swahili Amapiano Na "Kautaka"

Image Source: Online 

Siku za hivi karibuni kumekuwa na mjadala mkubwa kuhusu nani hasa ni mfalme wa Swahili Amapiano na wakati mjadala huo ukizidi kuwa wa moto, Jaivah ameamua kuchochea makaa na ngoma yake mpya ya kuitwa "Kautaka"

Ngoma ya "Kautaka" inakuja takriban miezi mitano tangu Jaivah aachie "Buruda" mkwaju ambao sio tu kwamba ulipelekea Jaivah kujulikana zaidi Tanzania lakini pia ulionesha kuwa kwenye uwanja wa Swahili Piano, Jaivah hashikiki. 

Kwenye ngoma yake mpya ya "Kautaka" Jaivah anachangia kipaza sauti na JF Music kutokea Afrika Kusini. 

Kimashahiri, Jaivah hana mengi ya kusema kwenye ngoma hii lakini bila shaka beat la ngoma hii na vibe lake kwa ujumla litakosha mashabiki mbalimbali. 

Tangu kuachiwa kwake, Kautaka imekuwa ni gumzo mtandaoni hasa Tiktok, kwani mashabiki wengi wameonekana kupenda kibao hiki ambacho ni kwanza kutoka kwa Jaivah kwa mwaka huu wa 2024.

https://youtu.be/7iB6btVU7rc?si=zpYx2NiFxnib3w6L

 

Leave your comment