Harmonize Aachia Ngoma Mpya Ya Kuitwa "Na Nusu"

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Baada ya ukimya wa miezi kadhaa hatimaye msanii kutoka Tanzania, Harmonize amerudi tena na ngoma mpya ya kuitwa "Na Nusu"

Mara ya mwisho kwa Harmonize kuachia ngoma mpya ilikuwa ni mapema mwaka huu alipoachia "I Made It" ambayo alimshirikisha Bobby Shmurda na Bien. 

Kwenye ngoma hii mpya, Harmonize anatoa sifa nyingi kwa wanawake kutokana ujasiri wao unaoonekana kwenye mambo mbalimbali. 

Harmonize kwenye kibao hiki ametumia mifano ya wanawake maarufu Tanzania ikiwemo wake wa Marais kama Maria Nyerere, Siti Mwinyi, Janeth Magufuli na wengineo wengi. 

"Na Nusu" imetayarishwa na B Boy Beats ambaye amehusika kutayarisha ngoma ya "Wote" ya Harmonize

https://youtu.be/5P2-dVxcQ44?si=xTJ90ceDvKL-423M

Leave your comment