Ngoma Mpya: Darassa Amvuta Zuchu Kwenye "Romeo"

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Baada ya ukimya wa miezi kadhaa, msanii nguli kutoka Tanzania Darassa ameamua kuunganisha nguvu na Zuchu kwenye ngoma mpya ya kuitwa "Romeo"

"Romeo" inakuja wiki chache tangu Darassa aachie ngoma yake ya kuitwa Confidence aliyofanya na Sheddy.

"Romeo" ni ngoma nzuri ya mapenzi ambayo ndani yake Darassa na Zuchu wanasifiana kwa kupeana maneno mazuri ya kimahaba.

Kwenye ngoma hii Zuchu ameleta sauti yake tamu na melody za kipwani wakati Darassa amepamba ngoma hii kwa mashahiri yake yaliyopangiliwa kwa ustadi mkubwa.

"Romeo" imetayarishwa na S2kizzy ambaye ni moja ya watayarishaji wakubwa wa muziki Tanzania, aliyehusika kutayarisha ngoma mbalimbali kama "Dah" "Mapoz" na "Shisha"

https://youtu.be/RCmOJTLi1k0?si=KhXjRtmIof8r6d3d

Leave your comment