Lava Lava Na Diamond Platnumz Kukutana Tena Kwenye "Kibango"

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Joto la burudani limeendelea kushamiri kunako lebo ya WCB na hii ni baada ya Lava Lava na Diamond Platnumz kudokeza ujio wa collabo mpa baina yao.

Lava Lava amedokeza ujio wa ngoma mpya baina yake na Diamond Platnumz ya kuitwa "Kibango" ambayo inatarajiwa kuingia sokoni hivi karibuni.

Lava Lava kupitia ukurasa wake wa Instagram amedokeza kuhusu ujio wa ngoma hiyo ambapo alidokeza kuwa ngoma itaingia sokoni hivi karibuni.

"Kibango" inatarajiwa kuwa ni collabo ya nne baina ya Lava Lava na Diamond Platnumz.

Wasanii hao wawili walishakutana kwenye ngoma tofauti tofauti ikiwemo "Jibebe" "Tuna Kikao" na "Far Away" 

Leave your comment