Diamond Platnumz Asikilizisha Mashabiki Kionjo Cha Ngoma Yake Mpya

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Wakati ngoma yake ya "Mapoz" ikiendelea kufanya vizuri, CEO wa WCB, Diamond Platnumz ameonesha nia ya kutaka kuachia ngoma mpya hivi karibuni.

Diamond Platnumz ameonjesha mashabiki zake kionjo cha wimbo huo akiwa jukwaani ndani wilaya ya Rufiji ambapo alikuwa akitumbuiza kwenye tamasha la muziki ambalo pia alikuwa amesindikizwa na wasanii wengine. 

Kwenye kionjo hicho, Diamond anaonekana akiwa anatumbuiza ngoma yenye mahadhi ya Amapiano ambapo pia kuna wasanii wengine wanaodhaniwa kuwa wameshirikishwa kwenye ngoma hiyo. 

Ikumbukwe kuwa mara ya mwisho kuachia ngoma ya Amapiano ilikuwa ni Julai mwaka jana alipoachia "Shu" ngoma ambayo Diamond alimshirikisha Chley Nkosi kutokea Afrika Kusini.

Leave your comment