Wasanii Kutoka Tanzania Walioshinda East Africa Arts Entertainment Awards (EAEA) Mwaka Huu

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Kiwanda cha muziki Afrika Mashariki kilisimama wima hivi karibuni na hii ni kufuatia hafla ya utoaji tuzo wa East Africa Arts Entertainment Awards

Kwenye tuzo za mwaka huu wasanii mbalimbali kutoka Tanzania waliondoka na ushindi mnono na kuandika historia mpya kwenye muziki

Rayvanny aliibuka kidedea baada ya kushinda tuzo tano kwa mpigo kupitia vipengele tofauti tofauti kama Mwandishi Bora Wa Mwaka na Msanii Bora Wa Kiume

Diamond Platnumz alishinda kipengele cha Best Overall Hitmaker huku Harmonize kupitia Single Again ameshinda kipengele cha Overall Hit Song Of The Year wakati Juma Jux akichukua ushindi wa Best Collaboration kupitia ngoma yake ya Enjoy. 

Lebo ya WCB Wasafi ilishinda tuzo ya Best Record Label huku producer wa lebo hiyo Lizer Classic alishinda kipengele cha Best Sound Engineer. 

Washindi wengine kwenye tuzo hizo kwa mwaka huu ni pamoja na S2kizzy ambaye ameshinda "Overall Hitmaker Producer Of The Year" huku Mr LG akishinda tuzo ya Producer Bora Chipukizi wakati DJ Joozey alishinda tuzo ya DJ Bora Chipukizi.

Leave your comment