Zuchu Azidi Kuwaburuza Tayla Na Yemi Alade Kwenye Mtandao Wa Youtube

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Msanii Kutoka Tanzania, Zuchu ameendelea kuandika historia kwenye muziki na hii ni mara baada ya kuwazidi wasanii wakubwa wa kike Afrika ikiwemo Tayla na Tiwa Savage kwa kuwa na wafuatiliaji wengi zaidi YouTube. 

Rekodi hii mpya inakuja siku chache tangu Zuchu  aweke rekodi ya kuwa msanii wa kwanza wa kike Afrika Mashariki kwa nyimbo yake ya "Sukari" kufikisha  views Milioni 100 

Akiwa na subscribers takriban Milioni 3.2 Zuchu anakuwa ni msani wa kike Afrika, Kusini mwa jangwa la Sahara kuwa na subscribers wengi zaidi kwenye mtandao waYouTube.

Kwenye rekodi hiyo, Zuchu anafuatiwa na Tayla kutokea Afrika Kusini mwenye subscribers Milioni 3.21 kisha Yemi Alade na Tiwa Savage kutokea nchini Nigeria. 

Leave your comment