Rayvanny Ashinda Tuzo Tano Kwenye East Africa Arts Entertainment Awards

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Msanii nguli kutoka Tanzania, Rayvanny hivi karibuni ameweka rekodi mpya kwenye muziki wake mara baada ya kushinda tuzo tano kwenye East Africa Arts Entertainment Awards maarufu kama EAEA

East Africa Arts Entertainment Awards ni tuzo zenye lengo la kuheshimisha wasanii na wadau waliopo kwenye sekta ya burudani Afrika Mashariki ambapo kwa mwaka huu tuzo hizo zilifanyika nchini Kenya.

Rayvanny amenyakua tuzo tano kwenye msimu huu wa East Africa Arts Entertainment Awards akiwa ni msanii ambaye ameshinda tuzo nyingi zaidi mwaka huu.

Rayvanny ameshinda kipengele cha Msanii bora wa kiume, Album au EP bora ya mwaka, Mwandishi bora wa mwaka, Best Lovers Choice Single and Best Inspirational Single.

Kwa ushindi huu Rayvanny anaungana na Diamond Platnumz, Harmonize na S2kizzy kwenye orodha ya watanzania walioshinda tuzo hizo kwa mwaka huu.

Leave your comment

Top stories

More News