Nyimbo Mpya: Diamond Platnumz Atuma Salamu Kwa Rais Samia Kwenye 'Namleta'

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Tangu aachie 'Mapoz' mapema mwezi Januari Diamond Platnumz ameamua kurudi tena na ngoma mpya ya kuitwa 'Namleta'.

Kwenye 'Namleta' Diamond Platnumz anamsifia Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa uchapa kazi wake huku akielezea namna ambavyo kiongozi huyo wa nchi anafanya mapinduzi ya kimaendeleo Tanzania.

Huu ni wimbo wenye vionjo vya Bongo Fleva ambao umepambwa na sauti tamu ya Diamond pamoja na vionjo vya muziki wa Congo kwenye beat.

Hii si mara ya kwanza kwa Diamond Platnumz kutoa wimbo ambao unamsifia Rais Samia kwani mwaka 2021 msanii huyo aliachia ya kumsifia Rais huyo ya kuitwa "Samia Suluhu"

Leave your comment