Rayvanny Ampa 'Hongera' Ex Wake Kwenye Ngoma Mpya

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Msanii nguli kutoka Tanzania, Rayvanny hivi karibuni ameachia ngoma yake mpya ya kuitwa "Hongera"

"Hongera" ni ngoma ya kwanza kutoka kwa Rayvanny kwa mwaka huu wa 2024 ikiwa ni nyinbo ambayo ameaichia takriban miezi minne tangu ashirikishwe na Dayoo kwenye Remix ya Huu Mwaka

Kwenye "Hongera" anatoa pongezi na sifa kedekede kwa mpenzi wake wa zamani ambaye kwa sasa anatarajia kupata mtoto na mwanaume mwingine.

Rayvanny ametumia ufundi mkubwa wa lugha pamoja miondoko ya Bongo kwenye kibao hiki ambacho mashabiki wengi wametafsiri kama ni ujumbe wa Rayvanny kwenda kwa mpenzi wake wa zamani, Paula ambaye kwa sasa ana ujauzito wa msanii wa Bongo Fleva, Marioo.

Ngoma hii imetayarishwa na Trone, producer nguli wa muziku kutoka Tanzania ambaye pia alihusika kutengeneza "Sukari" ya Zuchu.

https://youtu.be/ySPMS7vQZu8?si=rrpLqQa16Sj53OZ2

Leave your comment

Top stories