Chino Kidd Abadili Gia Angani Kwenye 'Binadamu'
12 April 2024
Image Source: Online
Writer: Charles Maganga
Chino Kidd kwa muda mrefu sasa amekuwa maarufu kupitia ngoma zake za Amapiano lakini kupitia ngoma yake mpya ya kuitwa 'Binadamu' msanii huyo ameonekana kubadilisha gia angani.
Chino Kidd ambaye pia ni CEO wa Wanaman Gang ameachia ngoma hiyo mpya ya kuitwa Binadamu ambayo amempa shavu Daway.
Kwenye 'Binadam' Chino Kidd anazungumzia kuhusu maisha yake ambapo humo ndani amejibu kuhusu tuhuma za kuwa na kiburi na dharau mara baada ya kupata ustaa.
Ukilinganisha ngoma hii na ngoma zake za awali kama Yesa, Nachange Vibe na Gibela, ni wazi kuwa kwenye Binadamu Chino ameamua kubadilisha aina yake ya muziki na kuiweka kando Amapiano.
Leave your comment