Ngoma Mpya: D Voice Arudi Kivingine Na 'Zoba'

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Baada ya ukimya wa takriban miezi mitano tangu aachie EP yake ya "Swahili Kid" msanii nguli kutoka Tanzania, D Voice ameachia ngoma mpya ya kuitwa Zoba

"Zoba" ni ngoma ya kwanza kutoka kwa D Voice kwa mwaka huu wa 2024 na inakuja ndani ya siku chache tangu msanii huyo adokeze ujio wa ngoma hiyo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Pamoja na kwamba D Voice anajulikana kwa miondoko yake ya muziki wa Singeli lakini kwenye Zoba, mkali huyo wa muziki ameamua kutumia Bongo Fleva laini kufikisha ujumbe wake.

Ndani ya "Zoba" D Voice anaielezea hadhira ni kwa namna gani amezama kwenye penzi la mwanamke ampendaye kiasi cha kurukwa akili.

Kimaudhui ngoma hii ya D Voice haina tofauti sana na "Zezeta" ya Rayvanny au "Teja" ya Lady Jaydee.

https://youtu.be/ltaVbcb46W0?si=86AFC15LBX7PJf9g

Leave your comment