Uchambuzi: Mimi Mars Aonesha Umalkia Wake Kwenye "Till I Die"

Source Image: Online 

Writer: Charles Maganga 

Mashahiri ya ngoma mpya ya Mimi Mars ya kuitwa "Till I Die" yanaweza yakawa mepesi lakini melody ya ngoma hiyo bila shaka inamuweka Mimi Mars kwenye kiwango cha juu kabisa.

Siku chache nyuma, Mimi Mars aliachia mkwaju wake wa kuitwa "Till I Die", ngoma kali ya mapenzi ambayo ndani yake Mimi Mars anaweka ahadi ya kuwa na mpenzi wake hadi mwisho wa maisha yake.

Kutokana na mahadhi ya ngoma hiyo, Till I Die bila shaka ni ngoma ambayo unaweza kuisikiliza ukiwa na mpenzi wako, ukiwa kwenye "vacation" au kwenye shughuli yoyote yenye mahadhi kama hayo 

Mashahiri ya ngoma hii ni mepesi na Mimi Mars bila shaka hakuonesha ufundi mkubwa kwenye mpangilio wa sauti lakini midondoko ya kwenye "Till I Die" kwa maana ya Melody itamfanya yoyote apende kusikiliza ngoma hii.

https://youtu.be/3-TrD_EW94w?si=2BByHjPwnMTDQbtT

Leave your comment