Jaivah Akutana Na Chley Nkosi Wa Afrika Kusini, Adokeza Ngoma Mpya

 

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Baada ya ukimya wa takriban miezi minne hatimaye nyota kutokea lebo ya Bxtra Records, Jaivah amedokeza ujio wake mpya hivi karibuni. 

Mara ya mwisho kwa Jaivah kuachia ngoma ilikuwa ni mwezi Desemba mwaka 2023 ambapo aliachia Buruda ambayo alimshirikisha Marioo, ngoma ambayo kufikia sasa imeshatazamwa takriban mara Milioni 3 kwenye mtandao wa YouTube. 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Jaivah alipost picha inayomuonesha akiwa na msanii kutokea Afrika Kusini, Chley Nkosi na kisha kudokeza kuwa ataachia ngoma mpya ya kuitwa Kautaka hivi karibuni. 

Chley Nkosi si jina jipya katika muziki wa Tanzania kwani msanii huyo kutoka Afrika Kusini tayari alishafanya collabo na wasanii wawili wakubwa kutoka Tanzania, Diamond Platnumz kwenye "Shu!" na Mbosso kwenye "Sele".

Leave your comment