Video Mpya: Mac Voice Aungana Na Director Kenny Kwenye “Niambie”

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Siku chache baada ya kuachia audio ya “Niambie” msanii nguli kutoka Tanzania, Mac Voice tayari ametimiza ahadi nyingine kwa mashabiki zake baada ya kuachia video ya “Niambie” 

Kwa wapenzi wa video za muziki zenye stori kali za mapenzi na zenye kusisimua basi video hii ambayo ni ya kwanza kwa Mac Voice kwa mwaka huu wa 2024 itakuwa ni burudani tosha kwao. 

Ukiweka kando ubora wa picha wa hali ya juu ambao umepamba video hii lakini pia namna ambavyo Mac Voice amevaa uhalisia, pia imechagiza video hii kuwa bora sana. 

Video ya “Niambie” imeongozwa na Director Kenny ambaye ni moja ya waongozaji video za muziki mahiri kutoka Tanzania ambaye pia ameshafanya kazi na wasanii tofauti tofauti ikiwemo Marioo kwenye “Sumu”, Zuchu kwenye “Sukari”, Rayvanny kwenye “Number One” na wengineo wengi

https://youtu.be/PGGcoNLL7pI?si=ZY52cvfLRFQCayd4

 

Leave your comment