Ngoma Mpya Tanzania Kwa Wiki Hii

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Hakuna kitu kinachowakosha wapenzi wa muziki wa Tanzania kama wasanii wao pendwa wakiwa ameachia nyimbo zao na kwa wiki hii wasanii mbalimbali kama kawaida ameachia ngoma mpya. 

Kutoka kwa wasanii kama Kontawa, Bruce Africa, Freshboys na wengineo wengi hizi hapa ni ngoma mpya Tanzania kwa wiki hii: 

 

Chegu - Kontawa Ft Billnass 

Kontawa ameachia Mkwaju wake mpya wa kuitwa Chegu ambao amemshirikisha Billnass na humo ndani Kontawa anazungumzia kuhusu maisha yake, vitu alivyopitia na mambo mengi tofauti tofauti. 

 

Emoji - FreshBoys Ft Bruce Africa 

Kundi la rap la FreshBoys limerudi tena na ngoma mpya ya mapenzi ya kuitwa Emoji ambayo inaunganisha ladha ya Bongo Hip Hop pamoja na vionjo vya Afrobeats ambavyo vimeongezwa na Bruce Africa.

 

Lalala - Bruce Africa Ft Mordecai Dex 

Wengi wanamjua Bruce Africa kwa uwezo wake wa kuandika ngoma nzuri za mapenzi na kwenye ngoma yake hii mpya Bruce kwa mara nyingine anathibitisha ubora wake kwa kumsifia mwenza wake huku alitumia maneno mazuri yaliyonogeshwa na sauti yake mujarab. 

Daddy - Kusah 

Utulivu, uandishi uliotulia pamoja na video kali yenye hadhi ya kimataifa ni kati ya sababu nyingi zilizopelekea ngoma ya Daddy kutoka kwa Kusah, ikiwa ni ngoma yake ya tatu kwa mwaka huu, kupokelewa vyema sana na mashabiki. 

 

Hip Hop Is Dead - Moni Centrozone 

Malume ameamua kuvunja ukimya na kuongea anayoyaona yanafaa kuhusu muziki wa Hip Hop kwani kupitia ngoma hii ametupa mawe gizani kuhusu mwelekeo wa muziki wa Hip Hop. 

 

 

 

 

Leave your comment