Diamond Platnumz Athibitisha Kushiriki Kwenye Albamu Mpya Ya Sholo Mwamba

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Mshindi mara tatu wa tuzo za MTV EMA, Diamond Platnumz hivi karibuni amethibitisha kuwa atashiriki kwenye albamu ya Sholo Mwamba ambayo iko mbioni kuingia sokoni. 

Sholo Mwamba hivi karibuni anatarajiwa kuachia albamu yake ya muziki na hivi karibuni Diamond Platnumz amethibitisha kuwa atakuwepo kwenye albamu ya msanii huyo mwenye miondoko ya Singeli. 

Katika kuonesha kuungana mkono albamu hiyo, Diamond Platnumz kupitia Insta story yake alidokeza kuwa ni lazima ashiriki kwenye albamu hiyo. 

“Mwamba The Rock. My Home Boy Brother, Love Always. Inshaallah Lazima Niwepo Kwenye Albamu Hiyo Mwanangu” aliandika Diamond Platnumz

Ahadi hii ya Diamond Platnumz inabidi kudhihirisha kuwa kwa sasa Diamond Platnumz ataendelea kufanya collabo na wasanii wa nyumbani baada ya hivi karibuni kufanya ngoma na Mr Blue, Jay Melody, Jux na wengineo wengi. 

 

Leave your comment