"Kila Kitu Tushakamilisha" Mbosso Athibitisha Ujio Mpya Wa Ya Moto Band

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Kama ulitamani kusikia tena, Ya Moto Band basi habari njema ni kwamba msanii kutokea lebo ya WCB, Mbosso hivi karibuni amedokeza kuwa huenda kundi hilo likaachia ngoma mpya hivi karibuni. 

Ya Moto Band ni kundi la muziki ambalo liliundwa na Mbosso, Aslay, Enock Bella na Beka Flavour ambalo lilianza mwaka 2013 na kisha kusambaratika mwaka 2016 baada ya wasanii wa kwenye kundi hilo kuanza kufanya kazi zao peke yao. 

Hivi karibuni, Mbosso ambaye mara tu baada ya kuachana na Ya Moto Band alisainiwa kwenye lebo ya WCB Wasafi amedokeza kuwa kuna mradi mpya wa kimuziki unapikwa na washiriki wa kundi hilo na kwamba muda si mrefu kundi hilo wataachia ngoma mpya. 

“Kila kitu tushakamikilisha, ni masuala ya kuyaweka sawa kati ya mimi na wenzangu, tunatoa (ngoma ya pamoja)” alizungumza Mbosso. 

Kipindi Ya Moto Band inafanya vizuri, kundi hilo lilitoa ngoma tofauti tofauti ikiwemo Nitakupwelepweta, Niseme, Mama, Cheza Kwa Madoido na nyinginezo nyingi. 

 

Leave your comment

Top stories

More News