Maua Sama Asimulia Alivyokatazwa Kutumia Kiingereza Kipindi Anaanza Muziki

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Nyota kunako kiwanda cha Bongo Fleva, Maua Sama hivi karibuni amesimulia namna ambavyo alikatazwa kuimba Kiingereza kipindi anaanza kuimba muziki. 

Maua Sama ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake ya Zamani, amesema kuwa wakati anatafuta nafasi ya kuimba, rapa Mwana FA alimpeleka kwa Marehemu Ruge Mutahaba ambaye alikuwa ni Mkurugenzi wa Uzalishaji Wa Vipindi Clouds Media. 

Kwa mujibu wa Maua Sama alidokeza kuwa alipofika aliambiwa aimbe na ndio hapo aliamua kuimba ngoma za Kiingereza ili kuonesha kipaji lakini baadae alishauriwa kwamba ili aweze kufanya vizuri kwenye muziki, Maua hana budi kuimba kwa kutumia lugha ya Kiswahili. 

“Ilikuwa tuko mimi, Mwana FA na Mheshimiwa January Makamba, tumeitwa pale, then he (Ruge) told me to sing. Nikaimba kwa kizungu pale. Then akaniambia hebu imba Kiswahili. Then nikaimba. Akaniambia kuna kazi ya kufanya but she is good” alizungumza Maua Sama 

 

Maua Sama aliendelea kwa kusema “Then baada ya hapo nikakatazwa kuimba kiingereza. Nikaambiwa kama unataka kutoboa kwenye muziki huu try to sing in Swahili” 

Tangu aingie kwenye muziki, Maua Sama ameweza kutengeneza hits tofauti tofauti ikiwemo Mahaba Niue, Sisikii, Iokote, Nioneshe na nyinginezo nyingi. 

 

Leave your comment