Ngoma Zinazofanya Vizuri Tanzania Kwa Wiki Hii

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Wakati mwezi February ukiwa unaelekea ukingoni, baadhi ya wasanii kutokea nchini Tanzania wameendelea kufanya vizuri kwenye majukwaa mbalimbali ya kusikiliza vizuri muziki ikiwemo kwenye mtandao wa YouTube. 

 

Kutoka kwa wasanii kama Diamond Platnumz, Zuchu, Nandy na wengineo wengi hizi hapa ni ngoma zinazofanya vizuri nchini Tanzania kwa wiki hii: 

 

Dharau - Ibraah Ft Harmonize 

Baada ya ukimya wa muda mrefu, Ibraah amerudi na ngoma yake mpya ya kuitwa Dharau. Ndani ya ngoma hii Ibraah na Harmonize wanaimba kwa hisia kali kuuonesha namna ambavyo hawapendi masimango na Dharau kwenye mahusiano. 

 

Mapoz - Diamond Platnumz Ft Jay Melody & Mr Blue 

Kwa wiki ya pili mfululizo, Mapoz ya Diamond Platnumz imeendelea kufanya vizuri YouTube ambapo kufikia sasa ngoma hiyo ambayo ni ya kwanza kutoka kwa Diamond Platnumz kwa mwaka huu wa 2024 imeshatazamwa mara Milioni 5.4 huko Youtube. 

 

Dah! - Nandy Ft Ali Kiba 

Kwa wapenzi wa ngoma za mapenzi basi Dah! bila shaka ni moja kati ya ngoma yao pendwa. Ndani ya wiki tatu tangu kuachiwa kwake, ngoma hii imeshatazamwa zaidi ya mara Milioni 6 kwenye mtandao wa YouTube 

 

Away - Marioo Ft Harmonize 

Usafi wa video, stori kali na uigizaji wa viwango vya hali ya juu wa Marioo kwenye video ya Away vimechagiza video hii kupendwa sana na mashabiki na kuwa kwenye orodha ya ngoma zinazofanya vizuri Tanzania kwa wiki hii. 

 

I Made It - Harmonize Ft Bobby Shmurda & Bien 

Ndani ya siku 10 tu tangu kuachiwa kwake, I Made It ya Harmo tayari imeshatazamwa zaidi ya mara Milioni 2.4 ikiwa ni video yake ya kwanza kwa mwaka huu wa 2024. 

 

Leave your comment