Zuchu Awapa Mashabiki Zake "Zawadi" Ya Video Mpya

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Baada ya kusubirisha mashabiki kwa siku kadhaa, hatimaye mshindi wa tuzo za Tanzania Music Awards kama msanii bora wa kike 2023, Zuchu ameachia video ya ngoma yake ya “Zawadi”. 

Video ya Zawadi inakuja takriban siku 12 tangu Zuchu aachie audio ya ngoma hiyo ambayo amemshirikisha msanii kutokea Comoros, Dadiposlim.

Zuchu na Dadiposlim walirekodi ngoma ya Zawadi mapema mwaka 2023 kipindi Zuchu ameenda kutumbuiza nchini Comoros 

Kwenye video ya Zawadi, Zuchu na Dadiposlim wanaonesha ushirikiano mzuri baina yao ambapo wawili hao anaonekana wakifurahi, kucheza na kushirikana pamoja kwenye video hii ambayo ni ya kwanza kutoka kwa Zuchu kwa mwaka huu. 

Video ya Zawadi imetayarishwa na Director Ivan ambaye ni mtayarishaji wa video za muziki kutoka Tanzania ambaye kufika sasa ameshafanya kazi na wasanii tofauti tofauti kutoka Tanzania kama Diamond Platnumz, Ali Kiba, Rayvanny na wengineo wengi. 

https://youtu.be/hevslIzA9nY?si=VLxTgsbRBwdZBwZT

 

Leave your comment